Niger, Mali na Burkina Faso zimetangaza kujitoa kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, wakiituhumu kushindwa kuwa chombo cha manufaa hasa katika kushughulikia hali dhaifu ya usalama kwenye kanda ya Sahel. Uamuzi wao wa kujitenga na ECOWAS una uzito gani? Rashid Chilumba amezungumza na mchambuzi ya siasa za Afrika, Mali Ali akiwa mjini Paris, Ufaransa.