1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchafuzi wa hewa uliuwa mamia ya maelfu ya watu katika EU

25 Novemba 2023

Maafisa wa Umoja wa Ulaya walikuta kuwa watu 250,000 walikufa katika mwaka wa 2021 kutokana tu na uchafuzi uliosababishwa na chembe chembe laini.

https://p.dw.com/p/4ZRAx
Watu 250,000 walikufa katika mwaka wa 2021 kutokana tu na uchafuzi uliosababishwa na chembe chembe laini barani Ulaya
Watu 250,000 walikufa katika mwaka wa 2021 kutokana tu na uchafuzi uliosababishwa na chembe chembe laini barani UlayaPicha: Marton Monus/REUTERS

Uchafuzi wa hewa uliuwa mamia ya maelfu ya watu katika Umoja wa Ulaya katika mwaka mmoja, kwa mujibu wa shirika la Mazingira la Umoja wa Ulaya - EEA.

Maafisa wa Umoja wa Ulaya walikuta kuwa watu 250,000 walikufa katika mwaka wa 2021 kutokana tu na uchafuzi uliosababishwa na chembe chembe laini.

Aina hii ya uchafuzi hutokana zaidi na magari yanayotumia gesi au viwanda vinavyotumia nishati ya makaa ya mawe.

Mbali na kupoteza maisha, watu wengi pia wanaugua magonjwa yanayohusiana na uchafuzi wa hewa. Wakati Ulaya ina hewa bora zaidi kuliko maeneo mengine ya dunia, bado haifikii viwango vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa.

Maafisa wa Umoja wa Ulaya wanataka iundwe sheria mpya za kuimarisha ubora wa hewa.