Uchaguzi nchini Kongo waingia siku ya pili
21 Desemba 2023Matangazo
Wapiga kura wanamchagua rais, wabunge na wajumbe wa serikali za mitaa. Rais aliyemo madarakani Felix Tshisekedi, anagombea muhula wa pili.
Upigaji kura ulicheleweshwa kwa kiwango kikubwa hapo jana, nchini kote.
Tume ya uchaguzi bado inajaribu kupeleka vifaa kwenye vituo vya kupigia kura vilivyopaswa kufunguliwa muda mrefu.
Kwa nini uchaguzi ni muhimu DR Kongo?
Mkuu wa tume ya uchaguzi (CENI) Denis Kadima, amesema kwenye televisheni ya taifa kwamba watu watapiga kura leo Alhamisi kwenye maeneo ambayo hayakuweza kupiga kura hapo jana.
Watu milioni 44 wamejiandikisha kupiga kura katika nchi hiyo yenye jumla ya watu milioni 100. Matokeo ya uchaguzi yatatangazwa baada ya siku kadhaa.