UChaguzi Nigeria
21 Aprili 2007LAGOS:
Uchaguzi nchini Nigeria ukiendelea sehemu nyengine, ulisimamishwa katika asehemu kubwa za jiji la Lagos ,kituo kikuu cha biashara kutokana na hitilafu katika karatasi za kupigia kura.Hii ni kwa muujibu wa maafisa wa Tume ya uchaguzi.
Uchaguzi nchini Nigeria tangu wa rais hata wa Bunge ulicheleweshwa kwa masaa 2 hii leo kwavile kura zilichelewa kuwasili kutoka Afrika kusini zilikochapishwa.Kituo kimoja cha TV kimearifu kuwa upigaji kura pia umesimamishwa katika sehemu mbali mbali za mkoa wa kusini wa River State.
Hapo kabla msemaji wa polisi huko Abuja,mji mkuu alisema polisi huko imezima jaribio la kukiteketeza kwa miripuko kituo kikuu cha Tume ya uchaguzi.Lori lililopakia gesi lilizuwiliwa kuripuka masafa mafupi tu kutoka jengo hilo.
Uchaguzi wa leo nchini Nigeria unatarajiwa kwa mara ya kwanza kukabidhi madaraka kutoka mkono mmoja wa rais wa kiraia kwenda kwa mwengine.
Watetezi wakuu katika uchaguzi huu wa dola lenye wakaazi wengi kabisa barani Afrika ni Umaru Yir’Adua anaeungwa mkono na rais Obasanjo,makamo rais Atiku Abubakar na kiongozi wa zamani wa kijeshi,Jamadari Muhammad Buhari.
Nigeria, ilinyakua uhuru wake kutoka Muingereza,1960.