1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa rais nchini Poland na Mvutano ndani CDU/CSU

25 Oktoba 2005

Kueemea Poland mrengo wa kulia kufuatia uchaguzi wa rais mwishoni mwa wiki na mbishano juu ya dai la waziri mkuu wa Bavaria, Edmund Stoiber kuhusu wizara anayopanga kuchukua katika serikali ya muungano-uchumi na teknolojia- ni baadhi ya mada kuu zilizohaririwa na magazeti ya Ujerumani leo hii.

https://p.dw.com/p/CHMS

Sasa inajulikana rasmi –Tume ya Uchaguzi nchini Poland imemtangaza mhafidhina mzalendo Lech Kaczynski mshindi na ndie ataekuwa rais mpya wa Poland.Likikosoa jinsi wapoland walivyopiga kura, gazeti la HANDELSBLATT linalotoka Düsseldorf ,laandika:

“Matokeo ya uchaguzi huo yamedhihirisha uhuru si lazima ufuatane na hisia za demokrasia.Imesadifu waliofanikiwa na kufunua macho,walionufaika na kufunua macho katika utaratibu wa mageuzi walitumia uhuru wao kutokwenda kupiga kura kwavile, hawakupendezewa na daraja ya wanasiasa waliogombea urais na hivyo waliwadharau.Wanaiona siasa kama kikwazo kinachowaharibia hadhi yao ya kunyayuka zaidi kimaisha.

Imetokea kwahivyo, hasa kwa kundi hili,matokeo ya uchaguzi ni pigo kwao, kwavile sasa wana uongozi wa dola ambao hawakuupendelea.Itakuwa kosa kubwa kutokana na matokeo ya uchaguzi huu kwa kambi ya magharibi na kwa Umoja wa Ulaya kuipa sasa mgongo Poland.”-hayo ni maoni ya Handelsblatt kutoka Düsseldorf.

Licha ya shaka shaka za Lech Kaczynski juu ya UU, gazeti la TAGESSPIEGEL kutoka Berlin linaonya kutomtilia shaka sana rais mpya: Laandika:

“Siku za nyuma licha ya misukosuko Fulani ya ndani nchini, Poland imedhihirisha nio mshirika wa kutegemeka.Ingelikuwa bora kwahivyo, majirani wa Poland wanachama wa UU kumkaribisha kiongozi huyo mpya licha ya wasi wasi wao juu yake.”

TAGESZEITUNG laandika kwamba Kaczynski ndio ni mwanasiasa apendae umaarufu,lakini ni mwerevu sana kutotambua kwamba, katika siasa za nje ni rahisi zaidi kubomoa kuliko kujeng aupya.Dai lake la malipo ya fidia kutoka Ujerumani kwa hasara ilizopata Poland katika vita vya pili vya dunia ni la kale kama lile la kudai kutungwa kwa sheria ya adhabu ya kifo.Dai lake la kutaka kuwekwa hesabu sawa laonesha limepokelewa uzuri na wapoland wengi.Msiba uliofuatia uasi wa mji wa Warsaw, 1944 na kuuwawa kwa wapoland 200.000 na kuteketezwa kwa mji wa warasw na manazi, haukusahaliwa hadi leo-latuzindua gazeti.

Likituchukua katika siasa za ndani ya Ujerumani,

gazeti la ABENDZEITUNG kutoka Munich lachambua mbishano uliozuka juu ya mamlaka yatakayotolewa kwa wizara ya uchumi ndani ya serikali mpya .

Laandika katika ugomvi wa wizara itakayoshikwa na Bw.Edmund Stoiber ,mwenyekiti wa CDU Bibi Merkel ametupa turufu yake yote mezani.Anawakera marafiki zake wachache aliobakia nao ……na hii haitatengeneza hali ndani ya chama.Wakosoaji ndani ya muungano wa CDU/CSU waliopo safu ya pili wamekereka kufungwa mdomo wao na Bibi Merkel katika kipindi hiki .

Kupitisha wakati hakutamsaidia kitu….”Lamaliza gazeti.

Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG lachambua sawa na hivyo linapoandika:

“Adhabu ya kwanza aliopata, ni matokeo yasiofurahisha ya uchaguzi.Adhabu ya pili, ni kuanza kwa kuchechemea bibi Merkel akiwa njiani kushika wadhifa wa ukanzela.Muungano wa vyama vya CDU/CSU unatoa sura ya kuingia serikalini bila kujitayarisha:Katika maswali ya nani ashike wadhifa gani hawaafikiani.Katika yale watakayo kuyatekeleza hakuna kinachofahamika. Na hii inakumbusha kidogo ilipoanza pia serikali ya muungano ya vyama vya SPD na Kijani .Wakati ule, chama cha CDU kiliviambia vyama hivyo ‘hamna muezalo.”