Uchaguzi wa Rais Pakistan
3 Oktoba 2007Pakistan,itakua na uchaguzi wa rais jumamosi hii ijayo.Katika uchaguzi huo,rais wa sasa- amirijeshi mkuu,jamadari Pervez Musharraf atagombea tena wadhifa huo akiomba kura za Bunge na mabaraza ya mikoa ili aweze kutawala kwa kipindi cha miaka 5 mengine.
Musharraf amesema yutayari kugawana madaraka na waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto,mradi tu chama cha bibi Bhutto kimejipatia viti vya kutosha katika uchaguzi wa bunge unaokuja.
Rais Musharraf ana uhakika mkubwa wa kushinda kwavile muungano wa vyama-tawala una wingi na zaidi ya wabunge 160 wa Upinzani wamejiuzulu na kuacha viti vyao Bungeni na katika mabaraza ya mikoa wakilalamika kupinga kugombea tena Musharraf wadhifa wa urais huku akisalia bado mkuu wa majeshi nchini Pakistan.
Rais nchini Pakistan, huchaguliwa sio na wapiga kura bali na wabunge wa mabaraza yote 2-moja likiwa na viti 342 na jengine 100 na wajumbe wa mabaraza ya mikoa 4 inayounda Pakistan:Punjab,Sindh,Mpaka wa kaskazini-magharibi na Baluchistan.
Jamadari Musharraf ameahidi kujiuzulu katika wadhifa wake wa mkuu wa majeshi baada ya kuapishwa kuwa rais tena wa Pakistan hapo Novemba 15.kipindi cha Bunge la sasa chamalizika kati ya Novemba mwaka huu.
Kwa desturi,marais nchini Pakistan, hawana turufu kubwa za uamuzi wa kisiasa ambazo kikawaida, hukabidhiwa wazirimkuu. Imedhihirika lakini mara nyingi na hata katika kipindi cha utawala wa jamadari Musharraf,katiba hubadilishwa kumpa rais madaraka zaidi.
Musharraf amejitolea kugawana madaraka na waziri mkuu wa zamani Bibi Benazir Bhutto anaepanga kurejea nyumbani kutoka uhamishoni mjini London mwezi ujao.
Serikali imebainisha jana kwamba iko tayari kumpa msamaha bibi Bhutto na hivyo kumfungulia njia ya kushiriki tena katika siasa za Pakistan.Sharti la kumshirikisha serikalini ni kwamba chama chake kijipatie viti vya kutosha.
Bibi bhutto alieondoka Pakistan 1999 kukwepa kile alichokiita “mashtaka ya kisiasa” dhidi yake ,ataongoza kikao cha halmashauri kuu ya chama chake mjini London hii leo kuzingatia mkono alionyoshewa na jamadari Musharraf.
Mahkama Kuu ya Pakistan ilibidi kuahirisha kikao chake kusikiliza mashtaka 2 mapya ya kumpinga
Jamadari musharraf kugombea tena wadhiofa wa urais.Yalitolewa na mawakili tangu wa kitaifa hata wa mikoa baada ya hakimu mmoja kujitoa akisema alikwisha elezea msimamo wake akiwa sehemu ya jopo la mahakimu 9 lililokataa malalamiko ya hapo kabla ijumaa iliopita ya kumzima Musharraf kugombea tena urais.