1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Uchaguzi wa Uturuki kufanyika Juni kama ilivyopangwa

22 Februari 2023

Serikali ya Uturuki inakusudia kufanya uchaguzi mkuu wa taifa hilo kama ulivyopangwa Juni 18, ikifutilia mbali wazo la kusogeza mbele kutokana na matetemeko mabaya ya ardhi yaliyolikumba taifa hilo mapema mwezi huu.

https://p.dw.com/p/4Nq0P
Belgien | Präsident Erdogan Türkei
Picha: Markus Schreiber/AP/dpa

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa maafisa watatu wa serikali walionukuliwa na shirika la habari la Reuters.

Wanasema kuna uwezekano mkubwa Rais Recep Tayyip Erdogan na mshirika wake wa chama cha kizalendo, Ally Devlet, watakutana kufikia makubaliano ya mwisho.

Soma zaidi: Tetemeko la ardhi na mwelekeo wa uchaguzi Uturuki

Siku chache baada ya matetemeko ya ardhi ya Februari 6, yaliyosababisha vifo vya watu 42,000, aliibuka afisa mmoja na kuonesha uwezekano wa kuwepo ugumu wa kufanya uchaguzi katika kipindi kilichokusudiwa.