1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UEFA EURO 2020 kuandaliwa kote Ulaya

7 Desemba 2012

Sasa ni wazi kwamba dimba la UEFA EURO mwaka wa 2020 litaandaliwa katika nch kadhaa za bara Ulaya. Kamati Kuu ya Shirikisho la Soka Ulaya UEFA kuidhinisha pendekezo hilo lake lililoanzishwa na Michel Platini

https://p.dw.com/p/16y7q
ITAR-TASS: KIEV, UKRAINE. JULY 1, 2012. The trophy (Cup) at the final match of the UEFA European Football Championship (Euro 2012 final), at the Olympic Stadium in Kiev. Spain defeated Italy 4 - 0. (Photo ITAR-TASS/ Artyom Korotayev)
Symbolbild UEFA Fußball Europameisterschaft 2020 EuropaPicha: picture-alliance/dpa

Platini alisema hatua hiyo ni njia moja ya kuepuka gharama nyingi wakati huu ambapo nchi nyingi za ulaya zinakumbwa na mgogoro wa kifedha. Katibu Mkuu wa UEFA Gianni Infantino amesema kinyang'anyiro hicho kitapewa jina “ A Euro for Europe”. Amesema hatua hiyo imekaribishwa na mashirika ya kandanda Ulaya isipokuwa tu na Uturuki. Hata hivyo mashabiki wengi wamezusha hisia mbalimbali wengine wakilalamika kuhusu gharama za usafiri kuhudhuria mechi katika nchi kadhaa. Wengine wanasema wazo la kutoandaliwa dimba hili katika nchi moja mwenyeji, litaharibu mazingira na msisimko wa tamasha hilo ambalo ndilo la pili kwa umaarufu baada ya Kombe la Dunia.

Dimba la UEFA EURO 2016 linatarajiwa kuandaliwa katika miji 10 kote Ufaransa lakini kuna tayari wasiwasi kuhusu maandalizi ya viwanja hasa vya mji wa kaskazini Lens na mashariki Lyon. Droo ya mechi za kufuzu kwa dimba hilo la mwaka 2016 itafaynwa katika mji wa Nice mnamo Machi 9, mwaka 2014. mechi za kufuzu kwa dimba hilo ambalo litapanuliwa kutoka idadi ya sasa ya timu 16 hadi 24 itaanza Septemba 2014 hadi Novemba 2015.

Rais wa UEFA Michel Platini UEFA ndiye aliyekuwa na wazo la nchi nyingi kuandaa dimba la EURO
Rais wa UEFA Michel Platini UEFA ndiye aliyekuwa na wazo la nchi nyingi kuandaa dimba la EUROPicha: AFP/Getty Images

Katika ligi ya soka hapa Ujerumani Bundesliga, viongozi Bayern Munich wanataraji kuipeleka hali yao nzuri ya Ligi ya Mabingwa katika kinyang'anyiro cha nyumbani Bundesliga wakati watakapoulinda uongozi wao wa pointi nane kileleni wma Ligi.

Bayern, baaday a kuwabwaga Bate Borisov nne kwa moja katikati ya wiki, watasafiri nyumbani kwa Augsburg katika mechi ya kwanza kati ya tatu ambazo ni lazima ishinde kabla ya wiki mbili za kipindi cha mapumziko ya msimu wa baridi. Mechi ya mwisho ya Bayern msimu huu wa 2012 ni dhidi ya Borussia Moenchengladbach, na kisha watakutana tena na Augsburg katika kombe la Shirikisho la Ujerumani awamu ya 16 tarehe 18 Desemba.

Nyuma ya Bayern katika ligi, kuna Bayer Leverkusen na pointi kumi na moja nyuma, na mabingwa watetezi Borussia Dortmund wanaonekana na waangalizi kama timu inayoweza kuwapiku Bayern na kunyakua taji. Dortmund wanakutana leo na VfL Wolfsburg.

Bayern Munich tayari wamefuzu katika awamu ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
Bayern Munich tayari wamefuzu katika awamu ya 16 ya Ligi ya Mabingwa UlayaPicha: Reuters

Leverkusen watacheza kesho Jumapili dhidi ya Hanover wakifahamu wazi kile ambacho Bayern na Dortmund watakuwa wamefanya Jumamosi. Schalke wako katika nafasi ya nne, pointi mbili nyuma ya Dortmund na pointi moja tu mbele ya Eintracht Frankfurt. Lakini Schalke wanacheza ugenini dhidi ya VfB Stuttgart baada ya kutosajili uhsindi katika mechi zao nne za mwisho za Bundesliga. Hoffenheim wako katika nafasi y 16 na watakutana na Hamburg.

Federer alenga Olimpiki Rio

Katika mchezo wa Tennis, Roger Federer anataka kushiriki katika michezo ya Olimpiki mjini Rio mwaka wa 2016 na atapunguza ratiba yake katika juhudi za kupata muda wa kutosha wa kujiandaa.

Mshindi huyo mara 17 wa Grand Slam atakuwa na umri wa miaka 35 wakati michezo ya Rio itakapowadia, lakini Mswisi huyo ambaye anaorodheshwa nambari moja ulimwenguni hajawahi kupata dhahabu katika Olimpiki, katika kitengo cha mchezaji mmoja kila upande, baada ya kushindwa na Andy Murray katika fainali ya Olimpiki jijini London mwaka huu.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters

Mhariri: Mohammed Khelef