1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa kusema "ndio" kwa Wapalestina UN

Admin.WagnerD28 Novemba 2012

Ufaransa imetangaza kuwa itaiunga mkono Mamlaka ya Wapalestina katika ombi lake la kutaka kuwa mjumbe mwangalizi asiyekuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa siku chache kabla ya kufanyika zoezi la kura ya maamuzi.

https://p.dw.com/p/16r1o
Picha: AP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Laurent Fabius amenukuliwa na Shirika la habari la Reuters akisema kuwa Alhamis au Ijumaa wiki hii, ombi hilo la Wapalestina litakapowasilishwa rasmi, Ufaransa itaunga mkono wakati wa kikao cha bunge la nchi hiyo.

Fabius amesema, "Na kwa kupitia majabdiiano baina ya pande zote mbili, tunataka suala la kuwepo taifa la Kipalestina litimie na kuwa kitu cha kweli".

Palestina imekuwa ikitafuta uungaji mkono wa mataifa ya Ulaya juu ya ombi lake hilo ikiwa ni hatua mojawapo ya kutaka kupata utambuzi mkubwa zaidi kwenye ngazi ya kimataifa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Laurent FabiusPicha: AP

Uhispania, Ureno zaunga mkono pia

Mbali na Uafaransa Uhispania na Ureno paia zimesema zitaliunga mkono takwa hilo la Palestina.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uhispania Jose Manuel Garcia Margallo aliliambia bunge jana kwamba Uhispania itaiunga mkono Palestzina kwasababu inahisi ndiyo njia muwafaka ya kuendeleza mwenendo wa amano

Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa inajiandaa kuendesha kura hiyo wiki hii ambayo kwa kiasi kikubwa inaungwa mkono na wanachama wengi wa umoja huo.

Licha ya matumaini waliyonayo Wapalestina akiwemo Rais wa Mamlaka hiyo Mahmoud Abbas ambaye atahudhuria kikao hicho maalumu Alhamis wiki hii, baadhi ya wajumbe katika umoja wa mataifa wameonya pia kuhusu matokeo ya hatua hiyo.

Balozi wa Wapalestina Riyad Mansour amesema kuwa kura hiyo ni hatua ya kihistoria kwa Wapalestina na hata Umoja wa Mataifa.

Wakati Wapalestina wakiendelea na juhudi hizo, Israel na baadhi ya washirika wake nao wameendelea kupinga uamuzi wa kuipa Malaka ya Wapalestina nafasi kama hiyo kwenye Umoja wa Mataifa.

Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas
Rais wa Mamlaka ya Wapalestina, Mahmoud AbbasPicha: picture alliance / dpa

Hofu ya Israel kupelekwa ICC

Kitendo cha maafisa wa Kipalestina kuhakikisha wanaimarisha mahusiano na nchi za ulaya kwa nguvu zote kadri iwezekanavyo kabla ya kura hiyo, kinaonyesha kuwa hawataingia mara moja kwenye mchakato mwingine wa kutaka utambuzi kwenye Mahakama ya Kimataifa Uhalifu, ICC.

Israel, Marekani na Uingereza ambazo zinapinga hatua hiyo ya Wapalestina kuingia kwenye taasisi za kimataifa , sasa zimeshtuka kuona kwamba haziwezi tena kuendelea kuzizima juhudi hizo. Sasa nchi hizo zinatafuta uhakika wa kwamba kama Wapalestina watajiunga kwenye ICC basi hawatoishitaki Israel kwenye mahakama hiyo.

Maafisa wa Kipalestina wamekana kuhusu suala hilo wakisema kuwa uamuzi wa kama wataomba nafasi kwenye mahakama hiyo au la, bado linabakia suala la ndani na muda ndio utakaoamua jambo hilo.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na Waziri wake wa Ulinzi Ehud Barak
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na Waziri wake wa Ulinzi Ehud BarakPicha: GALI TIBBON/AFP/Getty Images

Israel na Marekani zimeulaumu uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa zikisema kuwa njia pekee ya kuelekea kwenye taifa huru la Kipalestina ni kupitia mazungumzo ya amani. Hata hivyo mazungumzo hayo ya amani yamekwama kwa miaka miwili sasa kutokana na suala la makaazi ya walowezi wa Waisraeli kwenye Ukingo wa Magharibi ambao yameendelea kuongezeka licha ya kukemewa na mataifa mengi kuwa si halali.

Mwandishi: Stumai George/Reuters/ DPA

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman