1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa: Uchaguzi kukumbwa na idadi ndogo ya wapiga kura

Saleh Mwanamilongo
25 Juni 2021

Vigogo wa chama tawala wamejaribu kuwashawishi wapiga kura kujitokeza Jumapili kwa ajili ya duru ya pili ya uchaguzi mdogo nchini Ufaransa.

https://p.dw.com/p/3vZlv
Regionalwahlen in Frankreich | Wahlplakate
Picha: Bob Edme/AP/picture alliance

Kura ya maoni iliyochapishwa Alhamisi,inaonyesha kuwa ni asilimia 36 pekee ya wapiga kura watakaojitokeza kupiga kura Jumapili kwenye duru ya pili ya uchaguzi huo. Mbali na idadi ya watakaojitokeza uchaguzi huo umekumbwa pia na sintofahamu kwenye majimbo kadhaa.

Jumapili iliyopita chama cha mrengo wa kulia na chenye msimamo mkali cha Rassemblement National-RN cha Marine Le Pen, kilipata ushindi kwenye jimbo moja pekee la Kusini-Mashariki mwa Ufaransa. Ikiwa ni pigo kukwa kwa chama hicho kilichowavutia wapiga kura kwenye chaguzi zilizopita.

Marine Le Pen kiongozi wa chama cha RN cha mrengo wa kulia nchini Ufaransa
Marine Le Pen kiongozi wa chama cha RN cha mrengo wa kulia nchini UfaransaPicha: Jean-Paul Pelissier/REUTERS

 Chama tawala cha rais Emmanuel Macron cha Republique En Marche, kilipata pigo kubwa na kushindwa kupata asimilia 10 ya kura kwenye duru ya kwanza na hali bado huwenda ikawa hivyo kwenye duru hii ya pili. Kwa sasa chama hicho kimeshika nafasi ya tano kwa uwingi wa viti kwenye uchaguzi huo mdogo.

Nina kuibuka mshindi ?

 Swali kubwa hivi sasa nchini Ufaransa ni nani anayetarajiwa kupata ushindi kwenye uchaguzi wa hapo Jumapili? Bila shaka ni vyama vikongwe ambavyo vilipotea kwenye ramani ya siasa toka uchaguzi wa Macron mwenye msimamo wa wastani mwaka 2017.

Jean-Luc Mélenchon, kiongozi wa chama cha France Insoumise cha mrengo wa kushoto
Jean-Luc Mélenchon, kiongozi wa chama cha France Insoumise cha mrengo wa kushotoPicha: Getty Images/AFP/C. Simon

Kwa upande wake mgombea wa chama cha mrengo wa kushoto, kinachofahamika kama La France Insoumise Jean-Luc Mélenchon ambaye safari hii amedhirisha nia ya kugombea katika uchaguzi wa urais nchini Ufaransa amesema kuwa hatua ya kutofanikiwa kwenye uchaguzi mdogo wa hivi karibuni inaonyesha kuwepo mgawanyiko mkubwa kati ya wafuasi wa chama cha wanamazingira na chama chake, hali ambayo amesema inatoa mwanya kwa chama tawala cha La republique en marche kupata ushindi.