1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Ufaransa: Upo uwezekano wa suluhu ya mzozo wa Niger

28 Julai 2023

Viongozi waliofanya mapinduzi nchini Niger wameeleza kupata uungwaji mkono wa jeshi la nchi hiyo na kutoa wito wa utulivu

https://p.dw.com/p/4UV9N
Aserbaidschan l französische Ministerin für Europa und auswärtige Angelegenheiten Catherine Colonna in Baku
Waziri wa mambo ya nje ya Ufaransa Catherine Colonna, amezungumzia mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa huko Niger.Picha: Resul Rehimov/AA/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Catherine Colonna Ufaransa inaamini bado kuna uwezekano wa kuusuluhisha mzozo huo na kwamba Paris inaliona jaribio hilo la mapinduzi kama lisilokuwa na uhalali wowote.

Colonna ameongeza kuwa Rais Mohamed Bazoum yu bukheri wa afya na kwamba tayari amezungumza na Rais Emmanuel Macron.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ufaransa amesema Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, itaanda mkutano siku ya Jumapili ambao huenda ukajadili juu ya uwezekano wa viongozi waliofanya mapinduzi kuwekewa vikwazo na kwamba Ufaransa itaunga mkono vikwazo hivyo.