Ufaransa yaahidi euro milioni 100 kuisaidia Lebanon
24 Oktoba 2024Katika mkutano wa kimataifa wa kuisadia Lebanon, ulioandaliwa na Ufaransa, Rais Emmanuel Macron amesema msaada mkubwa unahitajika kuisadia nchi hiyo inayokabiliwa na mgogoro wa kiuchumi na watu milioni moja walioachwa bila makazi kutokana na vita.
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, amesema Umoja huo utatowa yuro milioni 20 mwaka huu kulisaidia jeshi la Lebanon na nyingine milioni 40 zitatolewa mwaka ujao.
Soma pia: Ufaransa yalenga kukusanya yulo milioni 500 kwa ajili ya Lebanon
Waziri Mkuu wa Lebanon, Najib Mikati, akizungumza pembezoni mwa mkutano huo wa Paris, ameshinikiza juu ya usitishwaji wa mapigano kati ya Israel na Hezbollah huku akisema hakuna kundi linalopaswa kuruhusiwa kubeba silaha nchini humo isipokuwa jeshi la taifa.