Ufaransa yachunguza mauaji
22 Machi 2012Rais Sarkozy pia amesema mtu yeyote nchini humo atakayepatikana akitembelea mara kwa mara mitandao inayounga mkono ugaidi ama kuchochea chuki au machafuko, ataadhibiwa kisheria. Rais huyo wa Ufaransa ameahidi kuanzishwa msako wa yeyote atakayekwenda katika nchi za kigeni kwa azma ya kupata mafunzo ya nadharia ya ugaidi.
Sarkozy alikuwa akizungumza baada ya mshukiwa wa mauaji ya watu 7 katika mji wa kusini wa Toulouse kupigwa risasi na polisi na kuuwawa baada ya mkwamo wa saa 32 wakati polisi hao walipojaribu kumkamata.
Mshukiwa huyo Mohammed Merah mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria, alishutumiwa kuwaua watoto watatu wa shule na mwalimu katika shule ya kiyahudi siku ya Jumatatu, pamoja na mauaji ya wanajeshi watatu wa Kifaransa mapema mwezi huu.
Mwandishi: Amina Aboubakar
Mhariri: Josephat Charo