1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Wanawake, watoto waregeshwa kutoka kambi ya itikadi kali

24 Januari 2023

Ufaransa imewarejesha nyumbani leo wanawake 15 na watoto 32 waliokuwa wanazuiliwa kwenye kambi ya wafungwa ya watuhumiwa wa itikadi kali nchini Syria.

https://p.dw.com/p/4Mdbv
Syrien Flüchtlingslager Roj
Picha: DELIL SOULEIMAN/AFP/Getty Images

Hayo ni kwa mujibu wa wizara ya mambo ya kigeni, ikiwa ni uhamishwaji wa tatu wa raia wa Ufaransa kutoka nchini humo.

Wanawake na watoto waliorejea Ufaransa leo walikuwa katika kambi ya Roj kaskazini mashariki mwa Syria chini ya utawala wa Kikurdi, karibu na mipaka ya Uturuki na Iraq.

Wamewekwa kwenye vituo vya huduma za jamii na mama zao watafikishwa mbele ya maafisa wa mahakama. Wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa imeishuruku serikali ya kaskazini mashariki mwa Syria kwa ushirikiano wake, ambao ulifanikisha operesheni hiyo.

Wakili Marie Dose wa jamaa za walioshikiliwa kwenye kambi kadhaa nchini Syria, amesema wanawake 150 na watoto walikuwa wanaishi katika kambi hizo kabla ya uhamishwaji wa leo.