SiasaAustralia
Ufilipino na Australia zasaini makubaliano ya ushirikiano
8 Septemba 2023Matangazo
Makubaliano hayo yalikamilishwa baada ya mkutano kati ya rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos na waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese aliekuwa ziarani mjini Manila.
Ziara ya Albanese iliyokuwa mwanzo wa mazungumzo ya pande mbili kati ya nchi hizo mbili ndani ya miaka 20, ilijiri baada ya misururu ya mikutano ya maafisa wa ngazi za serikali yake kuzuru Ufilipino tangu Marcos alipochukua madaraka mwaka 2022.
Chini ya ushirikiano huo wa kimkakati, nchi hizo zitapania kutanua ushirikiano wao katika Nyanja za ulinzi, usalama, tabia nchi na elimu.