1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfilipino

Ufilipino na China zafikia makubaliano kuzima mgogoro

21 Julai 2024

Ufilipino na China zimefikia makubaliano ya "muda" ambayo yanalenga kuzuia makabiliano katika mzozo wa eneo la Bahari ya Kusini ya China ambako kuna wanajeshi wa Ufilipino.

https://p.dw.com/p/4iYYY
Bahari ya Kusini ya China | Visiwa vya Spratly
Bahari ya Kusini ya China katika Visiwa vya SpratlyPicha: CPA Media/UIG/IMAGO

Katika taarifa yake Wizara ya mambo ya nje ya Ufilipino imesema makubaliano hayo yalifikiwa baada ya mfululizo wa mashauriano mjini Manila, kufuatia kuongezeka kwa mvutano katika eneo hilo.

Soma pia: Ufilipino yaishutumu China kutaka kupoka eneo la bahari

Taarifa hiyo imedokeza kwamba pande zote mbili zinaendelea kutambua hitaji la kuepuka mgogoro katika Bahari ya Kusini ya China na kukabiliana na tofauti zao kupitia mazungumzo na majadiliano na kwamba makubaliano hayo hayataibua chuki na kuathiri misimamo ya wengine katika eneo linalozozaniwa.

China, ambayo inadai karibu Bahari nzima ya China Kusini ni mali yake, imechukua hatua za kibabe katika eneo hilo katika miaka ya hivi karibuni ikizuia mataifa mengine kulifikia au kulitumia.