Leo imetimia miaka 35 kamili tangu lililokuwa kundi la waasi wa National Resistance Army, NRA lililopoukamata mji wa Kampala na kuipindua serikali iliyokuwepo nchini Uganda. Tangu wakati huo, tarehe 26 Januari 1986, Yoweri Museveni aliyekuwa kamanda wa NRA anashikiria madaraka ya urais Martin Oloo kutoka Kenya ni mchambuzi wa siasa anaitathmini miaka 35 ya utawala wa NRM.