1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Uganda yaondoa mchoro wa upinde wa mvua bustani ya watoto

2 Februari 2023

Maafisa nchini Uganda wametangaza kuondoa mchoro wa upinde wa mvua kutoka bustani ya watoto, kufuatia malalamiko miongoni mwa wazazi kwamba mchoro huo ni wa "kishetani".

https://p.dw.com/p/4N24O
Symbolbild Buthan LGBT
Picha: Micha Klootwijk/YAY Images/imago images

Maafisa nchini Uganda wametangaza kuondoa mchoro wa upinde wa mvua kutoka bustani ya watoto, kufuatia malalamiko miongoni mwa wazazi kwamba mchoro huo ni wa "kishetani" na unakuza vitendo vya ushoga katika taifa hilo lenye Wakristo wengi.

Katika taarifa iliyotolewa jana, Meya wa Entebbe, Fabrice Brad Rulinga alisema kwa miaka mingi, watoto wa Uganda wameufahamu upinde wa mvua kama tao zuri la rangi na kwa mujibu wa Biblia, unaakisi uzuri na heshima ya Mungu.

Lakini kwa bahati mbaya baadhi ya mavuguvugu yameamua kutumia upinde wa mvua kuwakilisha na kuakisi vitendo vinavyokwenda kinyume na mazoea ya waganda.

Emmanuel Mugabe, mwenyekiti wa chama cha wazazi nchini Uganda ameliambia shirika la habari la AFP kwamba rangi za upinde wa mvua katika mnara huo zilikuwa za kishetani na zinaashiria uvamizi wa ushoga kupitia ulaghai wa akili za watoto.