1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yaondoa ukomo wa umri wa rais

27 Julai 2018

Mahakama ya Uganda imehalalisha sheria inayoondoa ukomo wa umri kwa rais wa taifa hilo, hatua ambayo sasa inasafisha njia kwa rais Yoweri Museveni kuendelea kusalia mamlakani.

https://p.dw.com/p/32ATi
Yoweri Museveni | Gericht in Uganda ermöglicht Langzeit-Präsident Museveni weitere Amtszeiten
Picha: picture alliance/AP Photo/B. Chol

Mahakama ya Uganda imehalalisha sheria inayoondoa ukomo wa umri kwa rais wa taifa hilo, hatua ambayo sasa inasafisha njia kwa rais Yoweri Museveni kuendelea kusalia mamlakani.

Majaji wanne kati ya watano, miongoni mwa jopo la majaji waliosikiliza shauri hilo, walipinga baadhi ya vifungu vya sheria vya mabadiliko ya katiba yaliyofanywa mapema mwaka huu, yaliyoondoa kifungu kinachozuia mtu yoyote aliye na umri wa miaka 75 na kuendelea kugombea urais.

Museveni, ambaye hivi sasa ana miaka 73 na anayelindwa na mabadiliko hayo, asingeweza kugombea kwa awamu nyingine, wakati awamu yake ya sasa, ikifikia tamati 2021. Raia wengi wa Uganda wanapinga mabadiliko hayo.

Ingawa wakosoaji wa Museveni ambaye ni mshirika wa Marekani katika masuala ya ulinzi wa kikanda wakimtuhumu kwa kutaka kusalia mamlakani maisha yake yote, wafuasi wake wanasema ndiye mgombea bora zaidi katika uchaguzi ujao.