1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Uganda yaripoti visa vingine viwili vya Mpox

24 Agosti 2024

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha visa vingine viwili vya virusi vya homa ya nyani mpox na kuongeza idadi ya walioambukizwa kuwa watu wanne, katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

https://p.dw.com/p/4jsPc
Uganda yaripoti visa vingine viwili vya Mpox
Uganda yaripoti visa vingine viwili vya Mpox Picha: Moses Sawasawa/AP/picture alliance

Mkuregenzi Mkuu wa huduma ya afya nchini humo Henry Mwebesa aliliambia shirika la reuters kwamba, wagonjwa hao wawili wapya wanasemekana kuambukizwa kirusi cha Clade b1. 

Wagonjwa hao ambaye mmoja ni dereva wa lori kwa sasa wamewekwa karantini katika hospitali moja iliyoko Entebbe. 

WHO yatoa idhini kwa Gavi na Unicef kununua chanjo ya Mpox

Shirika la afya duniani WHO lilitangaza mripuko wa hivi karibuni wa Mpox kuwa dharura ya afya ya umma baada ya kirusi hicho kipya kinachodaiwa kuambukiza kirahisi na kwa kasi kugundulika.

Uganda iliripoti kisa cha kwanza Julai 24  wakati vipimo kutoka kwa maabara, vya wagonjwa wawili katika hospitali moja inayopakana na Jamhuri ya kidemkrasia ya Kongo kugunduliwa kuambukizwa homa hiyo.