1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhispania hatimaye yapata msaada

Sekione Kitojo10 Juni 2012

Hispania imepata msaada kutoka umoja wa Ulaya wenye thamani ya euro bilioni 100 kuzinusuru benki zake zinazokumbwa na matatizo , baada ya mazungumzo ya dharura na washirika wake wa eneo la sarafu ya euro.

https://p.dw.com/p/15BVP
JAHRESRÜCKBLICK 2011 - Old Greek Drachma coins that were replaced by Euro in 2002, in Athens, Greece 03 November 2011. The future of Greek Prime Minister George Papandreou_s government was in doubt Thursday as lawmakers from his governing Socialist party revolted against a referendum on whether the country wants to remain in the eurozone. Greek Finance Minister Evangelos Venizelos, who is also deputy prime minister, broke ranks with Papandreou on the idea of holding a referendum, insisting that the priority for the country was to remain in the eurozone. EPA/ORESTIS PANAGIOTOU +++(c) dpa - Bildfunk+++
Uhispania yaomba msaada wa fedha kwa mabenki yakePicha: picture-alliance/dpa

Baada ya mkutano uliotayarishwa kwa dharura kupitia mazungumzo kwa njia ya video , ambayo yamedumu kwa muda wa zaidi ya saa mbili siku ya Jumamosi, (09.06.2012) mawaziri 17 wa fedha wa kanda ya sarafu ya euro wametoa taarifa ikisema kuwa wako tayari kulishughulikia kwa njia nzuri , ombi la Hispania la kuomba msaada.

Makubaliano hayo, ambayo yamesifiwa na Ujerumani ambayo ndio injini ya uchumi wa Ulaya na Marekani pamoja na shirika la fedha la kimataifa , IMF, ni kielelezo cha Hispania kurejea matawi ya chini , ambapo serikali kadha nchini humo zimekuwa mara kwa mara zikipinga vikali haja ya msaada kutoka nje.

Serikali ya kihafidhina ya waziri mkuu Mariano Rajoy hatimaye imepiga magoti kutokana na mbinyo kutoka viongozi wa dunia , na muhimu zaidi , kwa masoko, ambayo yamesababisha gharama za kukopa nchini Hispania kupanda.

Spain's Prime Minister Mariano Rajoy answers questions from journalists regarding the government's latest economic measures during a join press conference with NATO's Secretary General, Anders Fogh Rasmussen, not seen, after a meeting at the Moncloa Palace, in Madrid, Thursday, April 26, 2012. (Foto:Daniel Ochoa de Olza/AP/dapd).
Waziri mkuu wa Hispania Mariano RajoyPicha: AP

Wakikaidi juhudi zote za wanasiasa, msaada wa mfuko wa eneo la euro sasa umesambaa katika uchumi wa nne mkubwa katika eneo hilo, ikiwa Hispania ni kubwa mara mbili ya eneo la Ugiriki, Ireland na Ureno kwa pamoja.

Serikali ya Hispania imetangaza nia yake ya kupata msaada wa fedha kutoka mataifa ya ulaya ili kuzipa mtaji benki zake ambazo zinahitaji msaada huo, amesema waziri wa uchumi Luis de Guindos katika mkutano na waandishi habari.

De Guindos amekataa kuelezea kuwa msaada huo kuwa ni makubaliano ya uokozi, ambayo serikali imekuwa ikiukataa hadi dakika za mwisho.

Spain's Economy Minister Luis de Guindos points during a news conference at the economy ministry in Madrid June 9, 2012. Spain's decision to ask for European aid for its banks reflected the commitment of all the members of the euro zone to their common currency, De Guindos said at a news conference on Saturday. REUTERS/Paul Hanna (SPAIN - Tags: BUSINESS POLITICS)
Waziri wa fedha wa Hispania Luis de GuindosPicha: Reuters

Hii haihusiani na uokoaji, amesisitiza, akidai kuwa msaada huo utaelekezwa kwa asilimia 30 ya mabenki ambayo yameathirika zaidi katika kuporomoka kwa masoko yanayohusika na mali katika mwaka 2008.

Makubaliano hayo hayaambatani na masharti katika uchumi jumla wa Hispania, na hakuna masharti ya kubana matumizi, de Guindos amesisisitiza.

Masharti pekee ni kwa mabenki, waziri huyo wa fedha amesema , akikiri hata hivyo kuwa makubaliano hayo yataongeza deni la Hispania ambalo linaongezeka.

Hata hivyo, mawaziri wa fedha wa eneo la Euro wamesema wanaimani kuwa Hispania itatekeleza majukumu yake ya kupunguza nakisi katika bajeti yake na kufanya mabadiliko katika uchumi wake. Hatua za maendeleo katika maeneo haya zitafuatiliwa kwa karibu na kufanyiwa mapitio kila mara, wamesema mawaziri hao katika taarifa.

The Bankia headquarters building is seen in Madrid, May 10, 2012. Hoping to put an end to a four-year banking crisis, Spain's government effectively took over Bankia SA, one of the country's biggest banks, late on Wednesday after days of market anxiety over the lender's viability. The centre-right government of Prime Minister Mariano Rajoy told Spaniards the banking sector was safe and said more measures to strengthen ailing lenders would come on Friday after a February banking reform proved insufficient. REUTERS/Paul Hanna (SPAIN - Tags: BUSINESS POLITICS)
Benki iliyokumbwa na matatizo ya BankiaPicha: REUTERS

Hispania ambayo itakuwa taifa la nne kutoka katika kanda inayotumia sarafu ya euro kupata msaada wa kifedha tangu kuzuka kwa mzozo wa madeni miaka miwili iliyopita , hatimaye imeomba msaada wakati gharama za kuzisaidia benki zikipanda katika wiki zilizopita.

Benki iliyotaifishwa hivi karibuni ya Bankia, ambayo imeathirika kwa kiwango kikubwa katika sekta ya nyumba , inahitaji kiasi cha euro bilioni 19 kuweza kuweka sawa mahesabu yake.

Chini ya makubaliano yaliyofikiwa Jumamosi, kiasi cha zaidi ya euro bilioni 100 zitatolewa na mfuko maalum wa uokozi wa Ulaya kuzipa mtaji benki za Hispania, wamesema mawaziri wa eneo la euro, wakitoa usaidizi muhimu kwa mahitaji yote yanayohitajika.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Bruce Amani