Uholanzi yataka kujiondoa mpango wa uhamiaji wa Ulaya
18 Septemba 2024Matangazo
Waziri wa Uhamiaji Marjolein Faber amesema katika mtandao wa X kwamba ameiarifu Halmashauri Kuu ya Umoja huo kwamba anataka nchi hiyo ijiondoe katika kanuni hizo za EU ili waweze kusimamia wenyewe sera zao za juu ya waomba hifadhi.
Serikali hiyo iliyo madarakani tangu mwezi Julai inayoongozwa na Geert Wilders inapanga kutangaza mgogoro wa kitaifa wa waomba hifadhi hali itakayoipa nafasi ya kudhibiti mipaka yake bila idhini ya bunge.
Hata hivyo, Umoja huo unatarajiwa kupinga nia hiyo ya Uholanzi kwa kuzingatia kuwa nchi wanachama wa Umoja huo ziliridhia makubaliano ya pamoja ya uhamiaji yaliyofikiwa mwezi Desemba mwaka 2023.