Taaluma ya uwandishi habari inazidi kuwa hatarini
3 Mei 2018Taaluma ya uwandishi habari inazidi kuwa hatarini, huku waandishi habari katika mataifa kama vile Syria na Yemen wakiwa waathiriwa wa makundi yanayohasimiana.
Wakati mwengine kazi yake inaweza kuwa hatarini, anakiri Husam. Raia huyo wa Syria, ambaye ni mwanaharakati anayekabiliana dhidi "ya utawala dhalimu wa Bashar al-Assad na dola la Kiislamu-IS"; katika mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter, amekuwa akituma video kutoka Idlib kwenye mitandao hiyo ya kijamii kwa miaka kadhaa sasa.
Hatua hiyo imemfanye alengwe. Mwaka 2015, alitekwa nyara na Jabhat al-Nusra, kikundi kilichochipuka kwenye kundi la al-Qaida, mwaka 2016. Alishikiliwa kwa siku 25, aliiambia DW kupitia WhatsApp, "kwa makosa ya kuwasiliana na majasusi wa Uingereza."
Waadishi wa Kujitegemea wanalengwa Syria
Hatimaye, aliachiliwa. Wengine hawana bahati : Yeyote anayeripoti kutoka Syria ni mlengwa wa makundi yanayokabiliana kwenye mzozo ambao umekuwepo kwa kipindi cha miaka saba. Wanahabari wa kujitegemea hutekwa nyara na kuuawa. Wachache huachiliwa huru. Raia wa Marekani James Foley na Steven Sotloff na Mjapani Kenji Goto pengine huenda wakawa wanahabari wa nje waliotekwa nyara chini Syria na kisha kuuawa kinyama. Wote watatu walikatwa vichwa, video ya mauaji hayo yakitumwa kwenye Youtube na Twitter na Dola la Kiislamu."
Kwa makundi yaliyo na itikadi kali, mauaji hayo huwa yanatumika kueneza propaganda, kwa mengine utekeji nyara ni biashara yenye kipato kikubwa.
Makundi yanayokabiliana hayajali wanahabari wa kujitegemea ambao hufichua uwongo na propaganda zao. Wanahabari wa Syria pia hulengwa, lakini vifo vyao mara nyingi havitangazwi Ulaya. Mwaka 2017 pekee, wanahabari tisa wa Syria waliuawa kwenye vita kwa mujibu wa Kamati ya Kuwalinda Wanahabari, mwaka huu wanne wameuawa.
Kuripoti kutoka Syria ni "kujitia kitanzi," Martin Durm ameiambia DW. Mwanahabari huyo wa Ujerumani anafahamu hili vizuri sana kutokana na tajriba yake. Mapema mwaka 2012, wakati wanahabari wa kigeni wangesafiri kupitia Syria, Durm alijipata katika mashambulio akiripoti kutoka Aleppo akiwa na mwenzake. Shirika lake la habari lilitaja shambulio hilo "lililowalenga."
Leo, ziara hiyo hawezekani, pengine katika baadhi ya majimbo ya Wakurdi yanayodhibitiwa na utawala wa Bashar al- Assad.
Ni vigumu kuthibitisha habari
Ziara ya mwisho ya Durm nchini Syria ilikuwa mwaka 2015. Tangu wakati huo, mara nyingi utawala umepuuza ama umekataa maombi ya hati ya kusafiri nchini humo. kama wanahabari wengi, analazimishwa kuripoti katika eneo ambalo haruhusiwi kufika ama akisafiri husafiri na jeshi la Urusi ama jeshi la Wakurdi
Mara nyingi wanahabari wanaopiga kambi jijini Cairo, Istanbul au Beirut, wanalazimishwa kukusanya habari ambazo wanaharakati kama vile Husam huwapa.
Lakini, Durm anaonya, ni "vigumu sana" kuthibitisha habari ama ripoti. "Wale walioko upande wa utawala pamoja na wale walioko upande wa upinzani — na leo, tuwe waaminifu, kiwango kikubwa cha habari zile ni za Wajihadi na waasi wa Kiislamu ambazo -hulenga kueneza propaganda."
Durm anaita "kampeini za kimakusudi za kupotosha" zinazofanywa na utawala pamoja na waasi. Lakini huku kukiwa na wanahabari wa kujitegemea kilomita nyingi kutoka Syria, utawala wa Assad unaweza kwa mfano kupinga madai ya matumizi ya mashambulio ya sumu katika mji unaoshikiliwa na waasi wilaya ya Duma mapema mwezi Aprili", anasema Durm.
Durm anashawishika kuwa hiyo ndio sababu ambayo hufanya mzozo wa Syria kupuuzwa na mataifa ya Ulaya kama usio na "umuhimu." Wengi, wangepanda kusahau mzozo huo kabisa.
"Hilo linachochewa na siri kuwa hatimaye Assad ashinde kwenye mzozo huo. Sio kwasababu yeye ni maarufu, lakini kwa sababu watu wanataka vita hivyo viishe." Anasema Durm akiwa shingo upande.
Mwandishi: Shisia Wasilwa, http://www.dw.com/en/war-reporters-the-great-silence/a-43591455?maca=en-rss_top_news-13961-xml-mrss
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman