1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhusiano kati ya Iran na Pakistan.

Halima Nyanza9 Machi 2009

Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari leo anaanza ziara nchini Pakistan kwa mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo juu ya Afghanistan na pia katika juhudi za kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/H8dc
Rais wa Pakistan, Asif Ali Zardari, kesho anaanza ziara nchini Iran katika juhudi za kuimariasha uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.Picha: pa / dpa

Hiyo itakuwa ziara ya kwanza ya Rais Asif Ali Zardari, wa Pakistan kuitembelea Iran tangu aliposhika madaraka mwezi Septemba mwaka uliopita.


Kwa mujibu wa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Pakistan, Abdul Basit, Rais Zardari atakutana na viongozi wa ngazi za juu wa leo na kesho atahudhuria mkutano wa kilele wa Shirika la Uhusiana wa Kichumi, ECO.


Mkutano huo utalenga juu ya jinsi gani shirika hilo ambalo lilianzishwa mwaka 1985 na Iran, Pakistan na Uturuki linaweza kukabiliana na mgogoro wa kifedha duniani.


Marais wa Afghanistan, Azerbaijan, Tajikistan na Uturuki pamoja na viongozi wa nchi nyingine katika kanda hiyo watahudhuria pia.


Shirika la Fedha duniani limekuwa likiisaidia Pakistan katika kuinua uchumi wake na mwezi Novemba mwaka uliopia iliidhinisha mkopo wa dola bilioni 7.6 kwa ajili ya kusaidia nchi hiyo katika matatizo ya malipo.


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Pakistan amesema mazungumzo kati ya Rais wa Pakistan na wa Iran Mahmoud Ahmadinejad yatalenga zaidi katika masuala ya kanda hiyo na dunia kwa ujumla, ikiwemo nchi ya Afghanistan ambayo imeharibiwa kwa vita.


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan amesema pia mazungumzo hayo yatalenga mradi wa dola bilioni 7.5 kwa ajili ya kusafirisha gesi ya Iran na kwamba ni nafasi kwa Pakistan kutumia ziara hiyo kuimarisha uchumi na mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.


Pakistan na Iran zilikubaliana mwaka jana mwezi Oktoba kuanzisha mradi bila ya kuishirikisha India, baada ya India na Iran kutofikia makubaliano mapya.


Wakati huo huo, Marekani ambayo ni mshirika mkuu wa Pakistan imesema Iran inaweza kualikwa katika mkutano wa kimataifa, baadaye mwezi huu kuelezea njia za kuboresha ujenzi mpya na demokrasia nchini Afghanistan na kumaliza mashambulio yanayofanywa na wapiganaji wa Kitaliban.


Iran inazingatia mwaliko huo kwa kusema kuwa shida zinazokumba jirani zao Aghanistan haziwezi kutatuliwa bila ya wao kuhusika.


Katika hatua nyingine, Pakistan imeisisitizia Iran kuisaidia Marekani na nchi nyingine katika kuiimarisha Afghanistan.


Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Pakistan Shah Mehmood Quresh amesema atazungumza na waziri mwenziye wa Iran kuhusu suala hilo.


Ameielezea Iran kama nchi muhimu katika kanda hiyo na kusema kuwa itakuwa vyema ikahudhuria mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje za Nje utakaofanyika Afghanistan Machi 31.


Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema katika mkutano huo wa ushirikiano wa Kiuchumi kwamba sera za kukalia ardhi na kujiingiza kwa mataifa ya nje katika eneo hilo la mashariki ya kati hazikuzaa matunda yoyote nchini Iraq na Afghanistan.