1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UIGE: Mripuko wa virusi vya Marburg nchini Angola

16 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFMf

Idadi ya watu waliofariki nchini Angola kutokana na mripuko wa virusi vya Marburg imefikia 230.Hiyo ni idadi kubwa kabisa ya vifo vilivyo sababishwa na virusi hivyo vilivyogunduliwa mwaka 1967 kwa mara ya mwanzo baada ya wafanyakazi kwenye maabara katika mji wa Marburg,kaskazini mwa Ujerumani kuambukizwa na nyani kutoka Uganda.Kiini cha mripuko wa virusi hivyo nchini Angola ni mji wa Uige ulio sehemu za ndani,kaskazini mwa nchi.Virusi vya Marburg vinaweza kumuuwa mtu mwenye afya katika kipindi cha wiki moja tu baada ya kuanza kutapika na kuwa na tumbo la kuendesha na hatimae kutokwa damu ndani kwa ndani.Kwa hivi sasa hakuna tiba ya virusi hivyo.