1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza na Marekani zajadili bishara huria

Ibrahim Swaibu
5 Mei 2020

Uingereza Jumanne imeanza mazungumzo ya biashara huria kati yake na Marekani baada ya taifa hilo kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/3bok1
Britische und Amerikanische Flagge
Picha: Getty Images/AFP/D. Leal-Olivias

Baadhi ya wanachama katika serikali ya cha Conservative cha Waziri Mkuu Boris Johnson wanatumai kuwa huenda Marekani na Uingereza zitafikia makubaliano ya biashara huria, wengi wao wakisema hatua hiyo itakuwa mojawapo ya manufaa ya Uingereza kwa kuondoka kutoka katika Umoja wa Ulaya.

Maafisa  wanasema  awamu ya kwanza ya majadiliano hayo itahusisha  masuala kadhaa; yakiwemo biashara ya bidhaa na huduma, biashara ya kidijitali, uwekezaji pamoja kuzisaidia biashara ndogo ndogo.

“Makubaliano hayo, yatafufua tena uchumi baada ya kulitokomeza janga la virusi vya korona,” balozi wa Marekani nchini Uingereza Woody Johnson amenukuliwa akisema.

Waziri  wa biashara ya kimataifa wa Uingereza Liz Truss amesema kuwa Marekani ni mshirika wao mkubwa,  na hivyo basi makubaliano yatasaidia chumi za mataifa hayo mawili kuimarika tena baada ya kuyumbishwa na athari za virusi vya Corona.

Truss na Robert Lighthizer, kwa pamoja watafungua mazungmuzo hayo kabla kuungana na maafisa  wengine ambao wataendelea na majadiliano hayo  kwa kipindi cha wiki sita.

Katika mwaka uliopita 2019, biashara kati ya Marekani na Uingereza ilitathminiwa kuwa na thamani ya yuro bilioni 220.9 sawa na dola bilioni 275. Serikali ya Uingereza imesema endapo makubaliano ya biashara huria  yatafikiwa, huenda biashara ikaongezeka kwa kiasi cha yuro bilioni 15.3.

Boris Johnson
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris JohnsonPicha: Getty Images/J. Mitchell

Mnamo mwaka 2016 Uingereza ilipiga kura ya maoni na kuamua kuondoka kutoka  Umoja wa Ulaya, hata hivyo baada ya mkangayiko wa kisiasa  taifa hilo lilijitoa mnamo Januari 31, 2020 na kuanza mazunguno ya biashara na mataifa menginie ikiwemo Marekani.

Uingereza bado iko katika kipindi cha mpito hadi Desemba 31, hali ambayo inalifanya taifa hilo bado kuwa na uhusiano na umoja huo ili kutoa muda kwa pande hizo  mbili kujenga uhusiano mpya. Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Ulaya wamesema kuwa huenda itakuwa vigumu kufikia makubaliano ya biashara kati ya Uingereza na umoja huo kufikia mwishoni mwa mwaka 2020.

Kumekuwa na wito wa kutaka muda wa kufikia makubaliano kuhusu biashara uongezwe kufuatia athari za janga la virusi vya corona,  lakini Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ambaye aliongoza kampeni ya taifa hilo kujiondoa kutoka katika umoja huo, kufikia sasa bado amekataa muda huo kuongezwa

Mwandishi: Ibrahim Swaibu

Mhariri: Buwayhid, Yusra

Chanzo: AFP