Uingereza na Ujerumani kushirikiana zaidi katika ulinzi
25 Julai 2024Hii ni kwa ajili ya kurejesha mahusiano na washirika wa Ulaya baada ya Uingereza kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya.
Katika ziara yake ya kwanza mjini Berlin, waziri wa ulinzi wa Uingereza John Healey ametia saini makubaliano na mwenzake Boris Pistorius ambayo yamesifiwa kuwa ya aina yake kati ya washirika hao wa jumuiya ya kujihami ya NATO.
Makubaliano hayo yanajumuisha kando na mambo mengine, ahadi ya kuimarisha sekta ya ulinzi katika nchi zote mbili, ushirikiano katika maendeleo na ununuzi wa silaha na kuratibu njia bora za kuisaidia Ukraine.
Pistorius amewaambia waandishi wa habari kuwa, makubaliano hayo yataimarisha pia nguzo ya Ulaya ndani ya jumuiya ya NATO.
Makubaliano hayo yanatokea wakati serikali mpya ya Uingereza, baada ya ushindi wa kishindo mwezi huu, inapojaribu kurejesha uhusiano wake na Ulaya.