UK na EU zapiga hatua katika biashara na Ireland Kaskazini
25 Februari 2023Matangazo
Hilo limedokezwa hii leo na waziri mkuu wa Ireland leo Varadkar ingawa amesema bado ni mapema kutabiri iwapo mkataba utapatikana ndani ya siku chache zinazokuja.
Mfalme Charles wa Tatu aapa kuendeleza mchakato wa amani wa Ireland Kaskazini
Hivi karibuni kumekua na mwelekeo wa kutia moyo unaolenga kupunguza ukaguzi mkali wa bidhaa kwenye mpaka wa Ireland mbili. Ukaguzi huo ni sehemu ya masharti ya kile kinachofahamika kuwa itifaki ya Ireland Kaksazini iliyofikiwa wakati wa mchakato wa Brexit.
Itifaki hiyo italazimisha kuwepo udhibiti mkali wa biashara kati ya Ireland iliyo mwanachama wa Umoja wa Ulaya na Ireland Kaskazini iliyo sehemu ya Uingereza ambayo iliyojotoa Umoja wa Umoja mwaka 2020.