1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuongeza doria mpaka wa Poland na Jamhuri ya Czech

27 Septemba 2023

Ujerumani yatangaza kuongeza doria mpaka wake na Poland na Jamhuri ya Czech, njia zinazotumika kusafirisha wahamiaji haramu.

https://p.dw.com/p/4Wsw9
Waziri wa Mambo ya Ndani Ujerumani Nancy Faeser
Waziri wa Mambo ya Ndani Ujerumani Nancy FaeserPicha: Maja Hitij/Getty Images

Ujerumani imetangaza leo mpango wa kuongeza doria ya polisi kwenye njia zinazotumika kuwasafirisha wahamiaji kinyemela kwenye mpaka wake na mataifa mawili jirani ya Poland na Jamhuri ya Czech. 

Hatua hizo mpya zimetangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Nancy Faeser akizitaja kuwa juhudi za kuzuia wimbi la wahamiaji kuingia Ujerumani kwa njia za magendo. 

Soma pia:Ujerumani: Watu wahama kutoka mijini kwenda vijijini

Hata hivyo waziri huyo hajaweka wazi idadi ya maafisa wa ulinzi watakaopelekwa kwenye eneo hilo la mipaka lakini amesisitiza hapataanzishwa vituo vya kudumu vya upekuzi.