Ujerumani kupeleka Kongo maabara ya kukabiliana na Mpox
21 Agosti 2024Matangazo
Wizara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo imesema leo kuwa pia kuna mipango ya kutoa mafunzo kwa wataalamu zaidi ili waweze kutambua dalili na kuufahamisha umma kuhusu hatua za kuzuia ugonjwa huo. Mafunzo sawa na hayo yaliandaliwa mwezi Juni mashariki mwa Kongo. Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani, Svenja Schulze amesema maafisa wa Afrika wameomba msaada kutoka kwa jumuia ya kimataifa. Kulingana na Schulze, msaada huo unapaswa kutolewa.Wakati huo huo, Kongo imeripoti zaidi ya visa vipya 1,000 vya homa ya Mpox katika wiki iliyopita hadi kufikia jana. Visa hivyo vipya vimeripotiwa wakati ambapo maafisa wa afya barani Afrika wakiomba chanjo zinazohitajika kusaidia kupambana na kitisho kinachoongezeka cha ugonjwa hupo katika barani Afrika.