UchumiUlaya
Ujerumani kukumbwa na mdororo wa uchumi 2023
9 Oktoba 2023Matangazo
Hii inaashiria kwamba Ujerumani - nchi yenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya - itaumaliza mwaka huu ikiwa katika mdororo wa uchumi.
Wakala wa takwimu nchini Ujerumani, Destatis, unasema pato jumla la taifa lilishuka kwa asilimia 0.2 mwezi uliopita baada ya kushuka kwa asilimia 0.6 mnamo mwezi Julai.
Soma pia:Ujerumani kubana matumizi katika bajeti yake mpya
Hali hiyo ya kuvunja moyo inatokana na kushuka kwa asilimia 6.6 kwenye nishati na asilimia 2.4 katika sekta ya ujenzi.
Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, limetabiri kuwa Ujerumaniitakuwa ndiyo nchi pekee kati ya mataifa yenye uchumi mkubwa barani Ulaya kuingia kwenye mdororo wa uchumi mwaka huu wa 2023.