1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yachangia dozi laki 1 za chanjo ya mpox

26 Agosti 2024

Ujerumani inatarajiwa kupeleka dozi 100,000 za chanjo ya mpox kwenye baadhi ya mataifa ya Afrika yaliyoathiriwa na ugonjwa huo wa homa ya nyani, amesema msemaji wa serikali, Steffen Habestreit.

https://p.dw.com/p/4jwKG
DR Kongo | Mpox mkoa wa Kivu Kusini
Mgonjwa wa mpox nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Picha: Ruth Alonga/DW

Amesema, Ujerumani pamoja na washirika wake wa Ulaya pia wataungana na Umoja wa Ulaya kujenga viwanda vya kuzalisha chanjo hiyo hukohuko Afrika, chini ya makubaliano ya muda mfupi ujao

Kulingana na taarifa iliyotolewa, njia itakayotumiwa kusafirisha chanjo hizo bado haiko wazi.

Serikali ya Ujerumani inasaidia mataifa yaliyoathirika kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kupitia Shirika la Afya ulimwenguni, WHO, kwa kutoa fedha na kupeleka wataalamu kutokea taasisi zake za wataalamu.