Ujerumani yahimiza juhudi za upatanishi Niger
4 Agosti 2023Baada ya ujumbe wa Jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS kuondoka patupu mjini Niamey na kushindwa kuirejesha madarakani serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.
Soma pia: Niger yavunja makubaliano ya kijeshi na Ufaransa
Urusi imesema hii leo kuwa uingiliaji wowote kutoka mamlaka zisizo za kikanda kama vile Marekani, hautotatua mzozo wa Niger. Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema Urusi inafuatilia kwa karibu hali hiyo na ina wasiwasi kuhusu mvutano unaoendelea katika eneo hilo.
Rais Mohamed Bazoum aliyepinduliwa madarakani ameitolea wito Marekani na Jumuiya ya kimataifa kusaidia kurejesha utulivu wa kikatiba. ECOWAS ambayo imewawekea vikwazo viongozi wa kijeshi imetishia uwezekano wa kuingilia kati kijeshi iwapo kufikia Jumapili hii, rais Bazoum hatorejeshwa madarakani.