Maelfu ya Watu kuandamana Ujerumani kupinga itikadi kali
27 Januari 2024Karibu waandamanaji 30,000 wanatarajiwa kuingia mitaani mchana huu katika mji wa Dusseldorf kukipinga Chama Mbadala wa Ujerumani, AfD, huku kukitarajiwa pia maandamano makubwa katika miji ya Aachen, Mannheim na Marburg na katika miji mingine.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius ataungana na waandamanaji katika mji wa Osnabrück huku Waziri Mkuu wa Jimbo la Saxony-Anhalt Reiner Haseloff naye akipanga kuungana na waandamanaji, huko Wittenberg.
Kunatarajiwa pia maandamano kesho Jumapili katika mji wa Hamburg na maeneo mengine. Sikju ya Ijumaa maelfu ya waandamanaji waliingia tena mitaani katika majiji ya Frankfurt, Saarbrücken, Herne na Gütersloh wakipinga itikadi kali za mrengo wa kulia.
Wizara ya Mambo ya Ndani imesema zaidi ya watu 900,000 waliandamana mwishoni mwa wiki iliyopita