1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yasema haitomtoa mwandishi Akhanlis kwa Uturuki

22 Agosti 2017

Baada ya mwandishi Dogan Akhanlis kukamatwa huko nchini Uhispania, Ujerumani yasema imefutilia mbali uwezekano wa kumkabidhi mwandishi huyo kwa Uturuki, hatua ambayo inaashiria msimamo mgumu wa Ujerumani kwa Uturuki.

https://p.dw.com/p/2ienU
Dogan Akhanli
Picha: picture-alliance/dpa/P. White/AP

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel ametoa wito wa kuungwa mkono raia wa Uturuki walio wengi ambao hawakumuunga mkono rais Recep Tayyip Erdogan. Ujerumani inazidi kuiwekea Uturuki msimamo wake mgumu.

Matamshi ya waziri Sigmar Gabriel yanaashiria ni jinsi gani uhusiano kati ya Ujerumani na Uturuki ulivyozorota.  Hasa baada ya rais Erdogan kuwataka raia wa Uturuki kutokuvipigia kura vyama vikuu vya Ujerumani katika uchaguzi wa Septemba na pia baada ya siku tatu tangu kukamatwa mwandishi Dogan Akhanlis huko nchini Uhispania. hatua ambayo inazua maswali juu ya shughuli za polisi ya kimataifa (Interpol)

Trauergottesdienst für Martin Roth in Berlin Gabriel
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Sigmar GabrielPicha: picture-alliance/dpa/J. Kalaene

Katika mkutano na waandishi  wa habari msemaji wa wizara ya mabo ya nje ya Ujerumani  Martin Schäfer alinukulu Ibara ya 3 ya Kanuni za Interpol, zilizowekwa na shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Lyon nchini Ufaransa. Kwa hiyo, kwa mujibu wa kanuni hiyo polisi ya kimataifa inawajibika kutoegemea upande wowote. Haya pia yanahusu masuala ya kijeshi, kidini au rangi. Msemaji huyo wa Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani Martin Schäfer amezungumza kwa kuzingatia hali ya sasa ya nchini Uturuki na amesema hafikirii kwamba mwandishi Akhanlis anaweza kurejeshwa Uturuki.

Kansela Angela Merkel

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliilaumu Uturuki siku ya Jumapili kwa kuitumia vibaya polisi ya kimataifa. Msemaji wa bibi Merkel, Steffen Seibert, alieleza kwamba inatia shaka jinsi Uturuki inavyoweza kuitumia polisi ya kimataifa kuwakamata watu wanaoikosoa serikali ya Uturuki akitolea mfano kukamatwa kwa mwandishi Akhanlis mwenye umri wa miaka 60 aliyekamtwa huko nchini Uhispania ilihali yeye si raia wa uturuki bali ni Mjerumani.  

Kimsingi, ni kwa busara ya kila nchi binafsi jinsi ya kukabiliana na miito kama hiyo ya kuwatafuta na kuwakama watu.  Kwa ujumla, nchi  190 wanachama wa Interpol wamekubaliana kuwepo  na taarifa za kutosha  katika kushughulikia maswala nyeti  yaliyopewa jina la  "taarifa nyekundu" au vilevile kuwe na aina nyingine ya  usaidizi. Hatua kama hii inatumika kwa kupambana na uhalifu wa kila aina, ikiwa ni pamoja na ugaidi.  Polisi ya kimataifa pia inashirikiana na Umoja wa Mataifa, kwa mfano, katika kufuatilia vikwazo bila ya kujali kama vinaelekezwa kwa watu binafsi, nchi au mashirika ya kigaidi.

Recep Tayip Erdogan hält Rede in Ankara
Rais wa Uturuki Recep Tayip ErdoganPicha: Reuters/U. Bektas

Je upo mkataba wa kimataifa?

Hakuna mkataba wa kimataifa. Kwa maneno ya kisheria, polisi ya kimataifa (Interpol) ni kama chama. Mabunge ya mataifa au taasisi nyingine za nje zote hazina uwezo wa kudhibiti kazi ya Interpol kwa kweli, ni zoezi la kimataifa na hufanyika kwa misingi ya nia njema.  Kuna mengi ya kufanya, orodha ya kesi zilizo katika "taarifa nyekundu" inayopatikana kwenye mtandao ina kurasa 17. Miongoni mwa wanaosakwa ni Wajerumani 15. Orodha nyingine iliyopo ni ile yenye kurasa 128 yenye majina na picha za watu ambao hawajulikani walipo iliyowekwa chini ya kifungu cha ''taarifa  ya rangi ya manjano''.

Maelezo maalumu ya Ujerumani yaliyopo katika polisi ya kimataifa ni ya  tangu Novemba 2014. Wakati Jürgen Stock alipochaguliwa kama Katibu Mkuu katika Mkutano Mkuu wa huko Monaco. Kabla ya hapo, alikuwa ni kaimu mkurugenzi wa polisi kitengo kinachoshughulikia uhalifu nchini Ujerumani (BKA) kwa miaka kumi. Tangu mwaka 2005, amekuwa mwanachama wa Bodi ya wakurugenzi wa polisi wa kimataifa na kamati kuu ya mwaka 2007 hadi 2010 kama Makamu wa Rais.

Mwandishi: Zainab Aziz/Fürstenau, Marcel

Mhariri:Josephat Charo