1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yasema mataifa mawili huru ndiyo suluhu pekee

22 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema suluhu ya mataifa mawili ndio njia pekee ya kusuluhisha mzozo wa sasa na itakayowezesha Waisrael na Wapalestina kuishi kwa amani.

https://p.dw.com/p/4bWvD
 Annalena Baerbock
Waziri wa Mambo wa Nje wa Ujerumani, Annalena BaerbockPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Baerbock amesema hayo mapema hii leo (Januari 22) kabla ya kuondoka kuelekea kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, mjini Brussels.

Amesema hata wale wanaoonyesha kutopendelea suluhu hiyo ya mataifa mawili hawajawahi luleta suluhu mbadala, huku akitoa mwito wa usitishwaji wa dharura wa mapigano katika Ukanda wa Gaza ili kuruhusu misaada ya kiutu.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja huo, Josep Borrel, pia amesisitiza juu ya suluhu ya mataifa mawili, na kuielezea Israel kabla ya mkutano huo kwamba haitaweza kuleta amani kwa mtutu wa bunduki.