Ujerumani yazitaka Iran, Hizbullah kutoishambulia Israel
2 Oktoba 2024Scholz alidai kuwa Iran inautishia ukanda mzima kuingia vitani na hili linatakiwa kuzuiwa kwa gharama yoyote ile na kuongeza kuwa Ujerumani na washirika wake wataendelea kuufanyia kazi mpango wa usitishwaji mapigano.
Naye Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alilaani kwa matamshi makali mashambulizi mapya ya kulipiza kisasi ya Iran dhidi ya Israel.
Soma zaidi: Israel yaapa kuendeleza mashambulizi kote Mashariki ya Kati
Macron alisema Ufaransa tayari "imekusanya" rasilimali zake za kijeshi kwenye eneo la Mashariki ya Kati ili kukabiliana na Tehran, huku akilionya kundi la Hizbullah kuacha kile alichodai ni "hatua za kigaidi dhidi ya Israel na watu wake".
Macron aliitaka pia Israel kusitisha mashambulizi ya kijeshi mara moja.
Huku hayo yakijiri, Israel inasema imeanzisha operesheni ya ardhini dhidi ya Hezbollah nchini Lebanon na kuwaamuru raia wa vijiji 24 kuondoka.