Ujerumani,Romani na Finland zapeleka msaada nchini Libya
13 Septemba 2023Matangazo
Halmashauri ya Umoja wa Ulaya imefahamisha kwamba msaada huo unaelekea katika mji ulioharibiwa vibaya wa Derna na jumuiya hiyo imeanzisha rasmi mpango wake wa kuwalinda raia ili kufanikisha shughuli za kutoa msaada.
Hatua ya Umoja huo wa Ulaya imechukuliwa baada ya mamlaka za Libya kutoa ombi rasmi la kutaka msaada jana Jumanne. Miongoni mwa msaada huo wa nchi za Umoja wa Ulaya ni pamoja na mahema,
Vitanda pamoja na mablanketi,jenereta,vyakula na mapipa ya maji. Kamishna wa Umoja huo wa shughuli za usimamizi wa migogoro Janez Lenarcic amesema jumuiya hiyo pia imetowa mchango wa awali wa yuro laki tano kama fedha za kusimamia shughuli za dharura.