1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Ujumbe wa China kuzuru Korea Kaskazini

7 Septemba 2023

Ujumbe wa China unakwenda Korea Kaskazini kuhudhuria maadhimisho ya miaka 75 ya kuanzishwa jamhuri

https://p.dw.com/p/4W2Rh
Nordkoreas seltsamste architektonische Wunderwerke
Picha: KIM Won Jin/AFP

Ujumbe wa chama cha kikomunisti cha China na serikali utakaoongozwa na naibu waziri mkuu Liu Guozhong utasifri kwenda Korea Kaskazini kushiriki sherehe za siku ya kuanzishwa kwa jamhuri Jumamosi wiki hii. Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la serikali KCNA iliyotolewa hivi leo,

Ziara hiyo inafanyika kufuatia mualiko wa kamati kuu ya Chama cha Wafanyakazi cha Korea WPK kinachotawala na serikali ya Jamhuri ya Demokrasia ya umma wa Korea DPRK. Korea Kaskazini inasherehekea siku ya kuasisiwa kwake Septemba 9 inayofahamika kama siku ya kuanzishwa kwa jamhuri na mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 75.