1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa EU wafika Goma kupambana na COVID-19 na Ebola

10 Juni 2020

Ujumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya umewasili katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kuunga mkono juhudi za kupambana na maradhi ya COVID-19 na Ebola.

https://p.dw.com/p/3dYnV
Brüssel EU Coronavirus Luftbrücke Demokratische Republik Kongo
Picha: picture-alliance/abaca/M. Thierry

Ujumbe huo pia unalenga kuhimiza upatikanaji wa suluhisho katika mizozo inayolikumba eneo hilo. Kabla ya kusafiri Goma, ujumbe huo ulifanya mazungumzo na rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi mjini Kinshasa.

Ujumbe huo unawajumuisha Janez Lenarcic, kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na usuluhishi wa mizozo pamoja na Jean Yves Ledrian akiwa ni waziri wa mambo ya nje wa ufaransa, ambaye ni kiongozi wa ujumbe huo. Akizungumza mjini Goma, Ledrian amesema kwamba watawasidia wakaazi wanaoendelea kukabiliana na janga la virusi vya corona  kote hJamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

Soma pia: Visa 56 vya COVID-19 kwenye gereza la kijeshi Congo

Baada ya kuwasili kwa ujumbe huo wawakilishi wengine wa Umoja wa Ulaya waliwasili mjini Goma wakiwa na vifaa  vinavyokuwa na uwezo wakusaidia kupungua maambukizi ya virusi vya corona na Ebola ndani ya maeneo yanayo athirika na majanga hayo.

Shehena ya misaada kutoka Umoja wa Ulaya kusaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Shehena ya misaada kutoka Umoja wa Ulaya kusaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Picha: picture-alliance/abaca/M. Thierry

EU kuipa DRC dola milioni 40

Wakati huohuo gavana wa mkoa huu wa kivu ya kaskazini Carly Nzanzu Kasivita akizungumza na vyombo vya habari alithibitisha kua umoja huo wa ulaya umeahidi kuitolea serikali ya Congo dola milioni 40 za marekani katika lengo lakusaidia kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa wa Corona.

Soma pia: Vita visivyokwisha vya ebola Congo

Kwa upande wao wakaazi mjini Goma wameonyesha hisia zao kwa kutoa maoni kuhusu msaada huo ulioletwa na wajumbe wa Umoja wa Ulaya. 

Haya yanajiri wakati huu ambapo raia waishio hapa kivu ya kaskazini wanaendelea kukabiliana na ugonjwa hatari wa Ebola huku idadi ya vifo ikiwa ni zaidi ya elfu mbili na wengine 53 walithibitishwa kuambukizwa na virusi vya corona tangu kutangazwa kwake hapa nchini jamuhuri yakidemokrasia ya Congo.

Mwandishi: Benjamin Kasembe/DW Goma

Mhariri: Daniel Gakuba