1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Waasi wa Houthi wa Yemen waenda Saudia kusaka amani

15 Septemba 2023

Ujumbe wa kundi la waasi la Kihouthi nchini Yemen umesafiri kuelekea Saudi Arabia kufanya mazungumzo na utawala huo wa kifalme.

https://p.dw.com/p/4WNAe
Mkuu wa Baraza la juu zaidi la Kisiasa la Houthi Mahdi al-Mashat alipokutana na ujumbe kutoka Saudi Arabia na Oman katika Kasri la Republican mjini Sanaa, Aprili 9, 2023.
Mkuu wa Baraza la juu zaidi la Kisiasa la Houthi Mahdi al-Mashat alipokutana na ujumbe kutoka Saudi Arabia na Oman katika Kasri la Republican mjini Sanaa, Aprili 9, 2023.Picha: SABA NEWS AGENCY/REUTERS

Mazungumzo hayo yananuia kumaliza vita vya miaka mingi kati ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia na waasi wa Kihouthi nchini Yemen, vita vinavyosambaratisha taifa hilo maskazini zaidi katika ulimwengu wa kiarabu.

Hata hivyo bado haijafahamika ni masharti gani yanayojadiliwa kati ya Saudi Arabia na waasi hao wanaoungwa mkono na Iran, ambao wameudhibiti mji mkuu wa Yemen wa Sanaa tangu Septemba mwaka 2014.

Ziara ya wajumbe hao inatokea baada ya wapinzani wa muda mrefu Saudi Arabia na Iran kufikia makubaliano ya upatanishi yaliyoongozwa na China mapema mwaka huu na kumekuwepo na shughuli kadhaa za kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.