1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine haitarajii kutafanyika mkutano wa pili wa amani

9 Oktoba 2024

Ofisi ya rais wa Ukraine Voloydmyr Zelensky imeonyesha mashaka juu ya kufanyika kwa kongamano la pili la amani kabla ya uchaguzi wa urais wa Marekani wa mwezi Novemba.

https://p.dw.com/p/4lYaD
Ukraine | Vita | Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Sergei Supinsky/AFP/ Getty Images

Ofisi hiyo imetwikwa jukumu la kuandaa kongamano hilo la amani ambalo linalenga kuwaleta pamoja viongozi wa dunia kujadili mipango ya Zelensky ya kuvimaliza vita kati ya Ukraine na Urusi.

Awali, Ukraine ilitaraji kuwa kongamano hilo lingefanyika kabla ya uchaguzi wa urais wa Marekani mnamo Novemba 5, japo baada ya mashauriano ya kina, ofisi hiyo imefikia uamuzi wa kutofanya kongamano hilo mwezi Novemba.

Soma pia:  Ukraine yashambulia bohari ya mafuta ya Urusi

Takriban viongozi 100 wa dunia na mashirika mengine yalihudhuria kongamano la kwanza la amani lililofanyika nchini Uswisi mwezi Juni, japo Urusi haikushiriki.