SiasaUkraine
Ukraine yaipiga meli ya Urusi kwenye rasi ya Crimea
26 Desemba 2023Matangazo
Ukraine inatuhumu kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba ndege zisizo na rubani kwa ajili ya matumizi ya vita vya Urusi nchini Kyiv.
Soma pia: Zelensky awasifu wanajeshi wake kwa kudungua ndege za Urusi
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Telegram jeshi la Ukraine limeishambulia meli hiyo kwa kutumia makombora katika eneo la Feodosia kwenye Bahari Nyeusi .
Soma pia: Ukraine yasherehekea Krismasi ya kwanza ya Disemba 25
Baada ya shambulizi hilo, Gavana aliyechaguliwa na Moscow, Sergei Aksyonov ameeleza kwamba mtu mmoja ameuwawa na watu wengine wawili wamejeruhiwa. Vile vile nyumba sita zimeharibiwa kwenye kadhia hiyo.