Ukraine yaonya kuwa Urusi inajaribu kuuteka mji wa Kupyansk
26 Novemba 2023Katika taarifa kupitia televisheni hii leo, msemaji wa jeshi la Ukraine Volodymyr Fityo, amesema wavamizi wa Urusi hawajafutilia mbali nia yao ya kuushambulia mji wa Kupyansk na kwamba wanataka kuukalia tena.
Vikosi vya Urusi vimeendeleza mashambulizi yao Kaskazini Mashariki mwa Ukraine katika wiki za hivi karibuni na kufanikiwa kuyadhibiti maeneo kadhaa.
Soma pia: Urusi yafanya mashambulizi makubwa mjini Kyiv
Mapigano sasa yanafanyika katika kijiji cha Synkivka, kilichoko kilomita chache Kaskazini Mashariki mwa Kupyansk.
Urusi ilifanya uvamizi kamili nchini Ukraine mnamo mwezi Februari mwaka 2022. Katika msimu wa vuli uliopita, Ukraine ilifanikiwa kukomboa sehemu kubwa ya eneo la Kharkiv ikiwa ni pamoja na makutano muhimu ya reli ya Kupyansk katika mto Oskil kama sehemu yake ya mashambulizi ya kulipiza kisasi.