SiasaUkraine
Ukraine yapambana kurudisha umeme baada ya mashambulizi
6 Desemba 2022Matangazo
Rais Volodymyr Zelensky amesema kati ya makombora 70 yaliyorushwa na Urusi mengi yalidunguliwa ingawa bado miundo mbinu ya nchi yake iliathirika kwenye matukio hayo.
Shirika la usambazaji umeme Ukraine, Ukrenegro limesema hatua mpya ya kuzimwa umeme imetangazwa katika maeneo yote ya nchi kutokana na athari zilizosababishwa na mashambulizi.
Hali hiyo inashuhudiwa wakati viwango vya joto vinateremka na baridi imeanza kuongezeka nchini Ukraine.
Rais Zelensky amesema wakati Urusi iliuchagua kufanya mashambulizi hayo unafungamana na nia ya nchi hiyo ya kutaka kusababisha uharibifu mkubwa kadri inavyoweza. Takriban nusu ya mfumo mzima wa nishati nchini Ukraine imeshaharibiwa.