1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Ukraine yasema haina nia ya kulikalia eneo la Kursk-Urusi

13 Agosti 2024

Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Ukraine, Heorhii Tykhyi, amewaambia waandishi wa habari mjini Kyiv kwamba nia ya nchi hiyo ni kuyalinda maisha ya watu wake.

https://p.dw.com/p/4jQUq
Ukraine | Urusi- Kursk
Raia wakiondolewa eneo la Kursk la Urusi kufuatia mapigano baina ya Ukraine na MoscowPicha: Alexey Belkin/NEWS.ru/globallookpress.com/picture alliance

Ukraine leo imesema haina nia ya kulikalia eneo la Kursk nchini Urusi. Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Ukraine, Heorhii Tykhyi, amewaambia waandishi wa habari mjini Kyiv kwamba nia ya nchi hiyo ni kuyalinda maisha ya watu wake.

Tykhyi vile vile amesema kwamba uvamizi mkubwa wanaoufanya kwa sasa utaipelekea mipango ya Urusi ya kijeshi kuparaganyika na kutoiwezesha nchi hiyo kutuma majeshi zaidi kupigana mashariki mwa Ukraine. Urusi yawaondoa raia wake kutoka eneo la Kursk

Ukraine inasema uvamizi huo umewapelekea kuchukua udhibiti wa kilomita elfu moja za mraba za ardhi katika eneo hilo la Kursk.Rais Volodymyr Zelenskiy amesema Urusi imekuwa ikilitumia eneo la Kursk kufanya mashambulizi ya makombora ndani ya Ukraine tangu mwezi Juni na kwamba jeshi la Ukraine limeyateka maeneo hayo.