MigogoroUkraine
Jeshi la Ukraine ladai kuharibu mifumo ya ulinzi ya Urusi
10 Juni 2024Matangazo
Kulingana na jeshi hilo mashambulizi hayo yalifanyika katika eneo la Dzhankoi, ambako yalisababisha "hasara kubwa" kwa ulinzi wa anga wa Urusi.
Hata hivyo, madai hayo hayakuweza kuthibitishwa mara moja na hakukuwa na maoni yoyote kutoka kwa wizara ya ulinzi Urusi.
Urusi imevurumisha mara kwa mara makombora ya masafa marefu kusini mwa Ukraine kutoka rasi ya Crimea ambayo Moscow waliikamata na kuidhibiti mwaka 2014.