1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yasema imevunja ngome ya "adui" huko Bakhmut

19 Septemba 2023

Ukraine imesema vikosi vyake vimefanikiwa kuvunja ngome ya ulinzi ya Urusi karibu na mji unaowaniwa wa Bakhmut ikiwa ni sehemu ya mashambulizi yake ya kujibu mapigo dhidi ya vikosi vya Moscow.

https://p.dw.com/p/4WUl3
Rais Volodomyr Zelensky wa Ukraine akiwa kwenye ziara huko Bakhmut
Rais Volodomyr Zelensky wa Ukraine alipowatembelea makamanda wanaongoza vita kwenye mji wa Bakhmut mwanzoni mwa mwezi Septemba Picha: Ukrainian Presidentia/Planet Pix/Zuma/picture alliance

Hayo yameelezwa na kamanda wa vikosi vya ardhini vya jeshi la Ukraine Oleksandr Syrskyi (siriski) ambaye amesema ushujaa wa askari wake umewawezesha kusonga mbele kwa "kuivunja ngome ya adui".

Taarifa hizo za mafanikio yanayozingatiwa kuwa muhimu kwa Ukraine, zimetolewa wakati rais Volodymyr Zelensky anajitayarisha kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa baadaye hii leo. Aliwasili Marekani jana ikiwa ni ziara yake ya pili tangu Moscow ilipoivamia nchi yake.

Amepangiwa pia kufanya mazungumzo na rais Joe Biden juu ya kile kiongozi huyo amesema ni "kuishukuru Marekani na serikali mjini Washington kwa kuiunga mkono Ukraine kupambania uhuru"