1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yashutumu 'uchaguzi bandia' wa Urusi nchini mwake

8 Septemba 2023

Ukraine imepinga kile ilichokiita “uchaguzi bandia” unaofanywa na Urusi katika majimbo yaliyonyakuliwa na nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4W7w4
Ukraine Krieg l Kommunalwahlen in der russisch kontrollierten Region Donezk l Stimmabgabe
Picha: Alexander Ermochenko/REUTERS

Kwenye taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Ukraine imesema chaguzi hizo za uongo ambazo Urusi inazifanya katika majimbo ya Donetsk, Lugansk, Zaporizhzhia, Kherson na Crimea, hazina thamani, huku ikiituhumu Urusi kwa kukiuka uhuru wa Ukraine.

Hayo yanajiri mnamo wakati  mashambulizi ya angani ya Urusi  yamewaua watu wanne na kuwajeruhi makumi zaidi kote nchini Ukraine.

Mashambulizi hayo yalilenga miji katika eneo la kati na mashariki mwa nchi. Waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine Igor Klymenko amesema raia watatu waliuawa eneo la Odradokamyanka na wengine kadhaa walijeruhiwa.