Ukraine yasikitishwa na kuvunjika uhusiano na Niger
8 Agosti 2024Niger ilichukua uamuzi huo siku chache tu baada ya nchi jirani Mali kuchukua uamuzi sawa na huo ikivituhumu vikosi vya Ukraine kwa kuyaunga mkono makundi ya waasi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Niger na Mali zinaendeshwa na serikali za kijeshi ambazo ziliingia madarakani katika mapinduzi ya karibuni na zimeigeukia Urusi na kundi lake la mamluki wa Wagner kwa msaada.
Wizara ya mambo ya kigeni ya Ukraine imesema katika taarifa kuwa inasikitisha kuwa maafisa wa Niger wamechukua uamuzi huo wa kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na Ukraine bila kufanya uchunguzi wowote kuhusu tukio la nchini Mali na bila kutoa ushahiri wowote kuhusiana na sababu za hatua ya aina hiyo.
Mali ilisema Kyiv iliwapa wanajeshi waasi taarifa za intelijensia, ambao kisha walizitumia kuwauwa mamluko kutoka kundi la mamluki wa Wagner na askari wa Mali kwenye uwanja wa mapambano mwezi uliopita wa Julai.